Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:19

Ukraine imetungua ndege 31 kati ya 34 zisizokuwa na rubani za Russia


Muonekano wa baada ya mashambulizi ya Russia huko Kharkiv
Muonekano wa baada ya mashambulizi ya Russia huko Kharkiv

Jeshi la anga la Ukraine limesema Jumamosi nchi hiyo inaendelea kujikomboa kutokana na mashambulizi ya Russia ya Ijumaa

Vikosi vya Ukraine vimetungua ndege 31 kati ya 34 zisizokuwa na rubani zilizorushwa usiku wa kuamkia leo na Russia, jeshi la anga la Ukraine limesema Jumamosi wakati nchi hiyo ikiendelea kujikomboa kutokana na mashambulizi makubwa ya Russia ya Ijumaa dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine.

Ndege hizo zisizotumia rubani zilitunguliwa katika maeneo ya kati, kusini na kusini mashariki mwa Ukraine, jeshi la nchi hiyo limesema. Wafanyakazi wa nishati bado wanafanya kazi ya kurejesha umeme kwa baadhi ya Ukraine, hata hivyo siku moja baada ya Moscow kuzindua kile Kyiv ilisema ni shambulio kubwa zaidi la vita kwenye gridi ya umeme ya nchi hiyo, mamlaka ilisema Jumamosi.

“Uwezekano wa kiufundi kwa usambazaji umeme” umerejeshwa katika mikoa iliyoathiriwa zaidi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Telegram. Lakini hali iliendelea kuwa ngumu katika eneo la Kharkiv, ambalo liliathirika sana.

Forum

XS
SM
MD
LG