Putin akiri hali ya maeneo manne ya Ukraine ambayo Russia imeyakamata ni tete

Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema Jumanne hali katika maeneo manne ya Ukraine ambayo alidai aliyakamata mapema mwaka 2023 ni ngumu sana.

Akizungumza na maafisa wa idara ya usalama ya Russia, Putin aliangazia maeneo ya Donetsk na Luhansk mashariki mwa Ukraine pamoja na Kherson na Zaporizhzhia upande wa kusini.

Rais wa Russia Vladimir Putin: “ Ningependa hasa kutaja vitengo vya idara za usalama ambavyo vimeanza kufanya operesheni katika mikoa mipya ya Russia. Ndiyo ni vigumu kwenu hivi sasa, hali katika jamhuri za Donetsk na Luhansk na katika mikoa ya Kherson na Zaporizhzhia ni ngumu sana.

Lakini watu wanaoishi huko, raia wa Russia wanawategemea nyinyi, kwa ulinzi. Ni wajibu wenu kufanya kila lilo muhimu kuhakikisha usalama wao, haki na uhuru kadri inavyowezekana. Kwa upande wetu, tutaendelea kuimarisha vitengo vipya vyenye vifaa vya kisasa na silaha na pamoja na maafisa wenye uzoefu.”

Rais Lukashenko

Kamanda wa majeshi ya pamoja ya Ukraine Serhiy Nayev amesema anaamini kwamba mkutano wa Putin na mwenzake wa Belarus utazungumzia uvamizi zaidi dhidi ya Ukraine


na kuhusika kwa kiasi kikubwa kwa majeshi ya Belarus katika operesheni dhidi ya Ukraine hasa kwa maoni yetu kuhusika pia huko kwenye eneo la mapambano.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amerejea kusema kuwa hana azma ya kupeleka wanajeshi wake ndani ya Ukraine, baada ya kuwapatia wanajeshi wa Russia sehemu ya kufanyia mashambulizi yao dhidi ya Ukraine mwezi Februari.

Russia haijawahi kuwa na udhibiti kamili wa maeneo yoyote manne ambayo yalikuwa sehemu ya madai ya Putin ya mwezi September kingilia katika maeneo hayo. Hatua ambayo imekataliwa na jumuiya ya kimataifa.