Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:10

Mji mkuu wa Ukraine washambuliwa na ndege zisizo na rubani za Russia


Wafanyakazi wa zima moto washughulika kuzima moto kwenye majengo mjini Kyiv, baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani, Oktoba 17, 2022. Picha ya AP
Wafanyakazi wa zima moto washughulika kuzima moto kwenye majengo mjini Kyiv, baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani, Oktoba 17, 2022. Picha ya AP

Utawala wa kijeshi mjini Kyiv leo Jumatatu umesema mji huo mkuu wa Ukraine umeshambuliwa na ndege zisizo na rubani za Russia, saa chache baada ya Rais Volodymyr Zelenskiy kutoa wito wake mpya kwa washirika wa Ukraine kuisaidia kuimarisha ulinzi wa anga katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Russia.

Majeshi ya Ukraine yalitungua ndege tisa zisizo na rubani zilizotengenezwa Iran, utawala wa kijeshi wa Kyiv umesema katika taarifa kwenye mtandao wa Telegram.

Russia mara kwa mara imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kuishambulia Kyiv na miji mingine ya Ukraine.

Zelenskiy alisema katika hotuba yake ya kila usiku jana Jumapili kwamba ulinzi wa anga ni “kipaumbele cha mara kwa mara” kwa utawala wake.

Zelenskiy alisema “Kwa kutusaidia kulinda anga zetu kikamilifu, kwa kutupatia mifumo ya kisasa zaidi ya ulinzi wa anga kwa idadi ya kutosha, mnaweza kuizuia serikali ya kigaidi kutumia zana zake kuu za ugaidi.”

XS
SM
MD
LG