Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:54

Ukraine inasema mashambulizi ya Russia yameuwa watu wawili huko Kherson


Mfano wa mashambulizi yaliyopita katika mji wa Kherson
Mfano wa mashambulizi yaliyopita katika mji wa Kherson

Waasi wanaoungwa mkono na Russia wamedhibiti sehemu za jimbo la Donetsk tangu mwaka 2014 na mapema mwaka huu eneo hilo lilikuwa sehemu ya unyakuzi uliotangazwa na Russia lakini likakataliwa na jumuiya ya kimataifa

Ukraine imesema mashambulizi ya Russia yamewauwa watu wawili Alhamisi katika mji wa kusini wa Kherson huku maafisa waliowekwa na Russia wakiripoti mashambulizi ya Ukraine katika mji wa mashariki wa Donetsk.

Kyrylo Tymoshenko naibu mkuu wa ofisi ya Rais Volodymyr Zelenskyy alichapisha kwenye Telegram kwamba mashambulizi ya Russia yalipiga jengo la utawala la mkoa huko Kherson.

Mjini Donetsk, meya aliyeteuliwa na Russia Alexei Kulemzin amesema mashambulizi ya makombora usiku wa kuamkia leo ni sawa na baadhi ya mashambulizi makubwa zaidi huko kwa miaka mingi.

Waasi wanaoungwa mkono na Russia wamedhibiti sehemu za jimbo la Donetsk tangu mwaka 2014 na mapema mwaka huu eneo hilo lilikuwa sehemu ya unyakuzi uliotangazwa na Russia lakini likakataliwa na jumuiya ya kimataifa.

Mjini Geneva, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk aliuambia mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu kwamba vita vya Russia dhidi ya Ukraine vinaendelea kukumbwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Turk ambaye alifunga ziara yake nchini Ukraine wiki iliyopita, alisema watu milioni 18 nchini Ukraine wanahitaji msaada wa kibinadamu na kwamba mashambulizi zaidi ya anga ya Russia "yanaweza kusababisha kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu na kusababisha watu wengine kukimbia makazi yao."

XS
SM
MD
LG