Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:14

Ukraine imenasa makombora kadhaa ya Russia yaliyoulenga mji mkuu


Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Kyiv, Ukraine Sept 8, 2022
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Kyiv, Ukraine Sept 8, 2022

Ukraine imesema kwamba imezuia shambulizi la Russia lililokuwa limeulenga mji wa Kyiv, huku mfumo wake wa ulinzi wa anga uliyapiga makombora 13 japo baadhi ya mabaki ya makombora hayo yameanguka na kuharibu majengo matano.

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschnko ameripoti kutokea milipuko katika wilaya ya Shevchenkivskyi katikati mwa Kyiv wakati wa shambulizi hilo la Jumatano mchana.

Hakuna vifo vya watu vimeripotiwa.

Mashambulizi ya Russia yanayotekelezwa na ndege zisizokuwa na rubani yamekuwa yakitokea Ukraine, pamoja na kuangushwa kwa roketi, makombora na mizinga mingine tangu mwezi Oktoba.

Mashambulizi yamekuwa yakilenga mifumo ya nishati na huduma ya maji, katika hatua ya kumaliza nguvu za raia wa Ukraine wakati msimu wa baridi kali unapoanza ulaya.

XS
SM
MD
LG