Maswali yaibuka kuhusu aliko Prigozhin, kiongozi wa mamluki wa Wagner

Mkuu wa kikundi cha wanamgambo wa Russia Wagner, Yevgeny Prigozhin akiwa kwenye paa la jengo la eneo lisilojulikana, tarehe 24 Juni 2023. Picha na @concordgroup_official / AFP

Maswali yaliendelea kuulizwa kuhusu aliko kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, licha ais wa Belarus Alexander Lukashenko, kusema Alhamisi kwamba hayuko tena Belarus na kwamba alikuwa amerejea nchini Belarus.

Prigozhin alikuwa ameenda Belarus kama sehemu ya makubaliano ya mwezi uliopita, ili kumaliza uasi wa muda mfupi, wa wa Juni 23, dhidi ya Rais wa Russia, Vladimir Putin, na maafisa wa ulinzi wa nchi hiyo.

Kikundi cha mamluki cha Wagner, kilikuwa kikilipwa na serikali ya Putin, kupigana pamoja na wanajeshi wa Russia nchini Ukraine, lakini mara kwa mara alilalamika kwamba Russia haikutoa silaha za kutosha kwa vikosi vyake.

Madai ya Lukashenko kwamba Prigozhin, aliyekuwa mwandani wa karibu wa Putin, alikuwa amerejea Russia, hayakuweza kuthibitishwa mara moja, na Kremlin ilikataa kutoa kauli yoyote juu ya mahali alipo Prigozhin.

Vyombo vya habari vya Russia, vimeripoti kwamba hivi karibuni, alionekana kwenye afisi zake, mjini St. Petersburg.

Rais Lukashenko alitupilia mbali mapendekezo kwamba Putin anaweza kuamuru Prigozhin auawe, akisema, "Ikiwa unafikiri kwamba Putin ni mkatili na mwenye kulipiza kisasi kummaliza, hapana, haitatokea."