Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:27

Rais wa Belarus amedai kwamba kiongozi wa Wagner amerudi Russia


Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin
Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amedai kwamba kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ambaye aliongoza jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa rais Vladimir Putin, yupo nchini Russia na wala sio Belarus.

Tangazo la Lukashenko linazua maswali zaidi kuhusu makubaliano kati ya Putin na Prigozin. Madai ya Lukashenko hata hivyo hayajabainishwa iwapo ni ya kweli.

Hakuna habari za kina kuhusu makubaliano kati ya Putin na Prigozhin, yanayoripotiwa kusimamiwa na rais wa Belarus.

Lukashenko alisema wiki ijayo kwamba kiongozi huyo wa mamluki alikuwa nchini Belarus.

Vyombo vya habari vya Russia viliripoti kwamba Prigozhin alionekana ofisi mwake mjini St. Petersburg, ishara kwamba huenda kulikuwepo na makubaliano ya kuendelea na shughuli zake nchini Russia.

Lukashenko ameambia waandishi wa kimataifa leo alhamisi kwamba kiongozi huyo wa mamluki alikuwa mjini St. Petersburg na kwamba mamluki wa Wagner walikuwa katika kambi zao. Hakutaja majina ya kambi.

Mamluki wa Wagner walikuwa wanasaidiana na wanajeshi wa Russia katika vita vinavyoendelea mashariki mwa Ukraine kabla ya kutokea jaribio la mapinduzi. Pia, wana kambi nchini Russia.

Lukashenko amesema kwamba Prigozhin amerejeshewa pesa na silaha zilizokuwa zimechukuliwa na maafisa wa Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG