Katika mahojiano na kipindi cha televisheni Jumapili “Fox News Sunday,” Pompeo hajasema ni nchi gani zilizo ruhusiwa na Marekani kukiuka vikwazo hivyo kwa kuendelea kununua mafuta kutoka Iran.
Amesema kuwa zilizo ruhusiwa ni nchi nane ambazo hazijatajwa majina “tunahitaji muda kidogo zaidi kufikia idadi ya sifuri.”
Pompeo amesema kuwa pamoja na kuondolewa vikwazo hivyo kwa kuruhusu nchi hizo kununua mafuta, “ vikwazo hivi dhidi ya Iran tayari vimekuwa na athari kubwa.
Rais Donald Trump aliiondosha Marekani mwaka 2018 kutoka katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yalioridhiwa 2015. Vikwazo hivyo vitaanza kutekelezwa Jumatatu.
Pompeo amesema sera ya Trump ya “ kuweka shinikizo la juu kabisa dhidi ya Iran itaendelea kufanya kazi kikamilifu kuanzia kesho.”