Mahakama ya juu ya nchi hiyo wiki iliyopita ilitoa hukumu hiyo kwa Zuma na kumwamrisha kufika jela ifikapo Jumapili jioni ili aanze kutumikia kifungo hicho.
Kulingana na taarifa ya mahakama Zuma asipofanya hivyo polisi wameambiwa wamkamate mnamo siku tatu zitakazo fuata.
Lakini Zuma siku ya Ijumaa aliwasilisha maombi ya kusitishwa amri ya kukamatwa kwake ambalo litakalosikilizwa siku ya Jumanne mahakamani.
Zuma mwenye umri wa miaka 79 ameiomba mahakama ya katiba kutafakari upya na kufuta uamuzi wake wa kumweka jela.
Mambo hayo yatasikilizwa Julai 12.
Akizungumza Jumapili usiku kutoka nyumbani kwake kiongozi huyo wa zamani amesema hatajisalimisha kwa polisi mwenyewe kwa muda uliyowekwa kwa sababu anasubiri uamuzi wa mahakama.