Wakaazi wenye hasira kutoka Hosteli ya Diepkloof katika kitongoji cha Soweto mjini johanesburg Afrika kusini, wamechoma matairi katika jaribio la kuziba barabara na kuwarushia mawe polisi kufuatia maandamanao ya ghasia ya kupinga ukosefu wa usambazaji wa huduma muhimu na hali mabaya ya makazi.
Polisi walijibu kwa kutumia mipira ya maji na risasi za mpira.
Shandu mmoja wa wakazi wa hosteli hiyo alisema,
“hakuna anayetushughulikia sisi kwa umakini’ Imebidi tuzibe barabara ili mambo yawe sawa. Kwa nini iwe hivi?”
Naye Sibongiseni Khoza kiongozi wa DIEPKLOOF hostel alisema,
“hapa kama mtu inabidi aende maliwato , inabidi amsubiri mwingine anayetumia. Suala la maliwato ni moja ya mengine makubwa ambayo yanatusumbua,”
“Namaanisha hii Afrika kusini ambayo tunasema iko huru bado kuna watu ambao wamedhulumiwa na kukandamizwa kwa njia hii, kwa kweli hosteli bado zimekandamizwa vibaya sana” aliongeza.