Siku ya Alhamisi baada ya moto kutokea kwenye njia kuu ya kusambaza umeme, ilisababisha umeme kukatika kote katika taifa hilo.
Waziri wa nishati Adebayo Adelabu, alisema moto ulisababisha mlipuko kwenye njia ya usambazaji umeme inayounganisha mitambo ya Kainji na Jebba katika jimbo la kaskazini la Niger, na kutegua gridi ya taifa.
"Moto huo umedhibitiwa kabisa na zaidi ya nusu ya
Njia za kuungaisha sasa zinafanyakazi na muda mfupi ujao huduma kamili zitarejeshwa kote," Adelabu alisema katika taarifa.
Uzalishaji umeme ulishuka hadi sifuri katika nyakati za asubuhi na kupanda tena baadaye hadi megawati 273, lakini kiwango hicho bado ni chini ya wastani wa usambazaji wa siku wa Megawati 4,100, data kutoka kwa Kampuni ya Usambazaji ya Nigeria (TCN) ilionyesha.
Usambazaji wa umeme wa gridi ya taifa umekuwa ukisuasua nchini Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkubwa ya mafuta na gesi, na kuzilazimisha kaya na biashara kutumia dizeli na mafuta kwa ajili ya majenereta.
Mwaka 2022 , Gridi hiyo ya umeme imeshindwa kufanya kazi angalau mara nne, ambapo mamlaka zimekuwa zikilaumu matatizo ya kiufundi.
Nigeria ina MW 12,500 za uwezo uliowekwa lakini inazalisha
takriban robo ya kiwangio hicho. Rais Bola Tinubu ameahidi kuboresha usambazaji kwa kuruhusu serikali za majimbo kujenga mitambo yao ya kuzalisha umeme kwa nia ya kusaidia kuchochea ukuaji duni wa uchumi.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters