Hatua hii imechukuliwa wakati maambukizi ya kirusi cha Omicron kinachosababisha COVID-19 yakiongezeka kwa wafanyakazi wake wa ndege na wafanyakazi wengine.
Shirika la ndege la United lenye makao yake Chicago lilifuta safari120 za ndege Ijumaa, wakati Delta lenye makao yake Atlanta limesema limefuta safari takriban 90.
Wote wamesema walikuwa wanafanyakazi kuwasiliana na abiria ili wasikwame katika viwanja vya ndege.
Hata hivyo Delta imesema imetumia njia zote mbadala na rasilimali ikiwemo kubadilisha njia za safari za ndege na wafanyakazi kwa ajili ya kuziba nafasi kwenye ratiba kabla ya haijafuta safari za ndege karibu 90 hivi leo.
Delta imesema sababu ya kufuta safari hizo ni kutokana na hali ya hewa na matokeo na maambukizi ya Omicron .