Maji katika Ziwa Tanganyika yameongezeka na kusababisha mafuriko katika bandari ya Bunjumbura, biashara zimevurugika katika mji mkuu wa kiuchumi na katika maeneo mengine yanayotegemea kwa kiwango kikubwa msaada kutoka wafadhili.
Raia wa Burundi walikuwa wakihangaika kukabiliana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo, huku maelfu ya watu wakikosa makazi na nyumba nyingi na shule kuharibiwa.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa tangu Septemba zaidi ya watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko kufuatia hali mbaya ya hewa ya El Nino.
Serikali imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia katika kukabiliana na hali hiyo mbaya.
Nchi za Tanzania na Kenya zimeshuhudia zaidi ya vifo 50 na maelfu kukoseshwa makazi kutokana na mafuriko yaliyoathiri kanda hiyo.
Baadhi ya habari hii inatoka shirika la habari la AP