Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:58

Shule kufunguliwa tena Sudan Kusini baada ya kufungwa kutokana na joto kali


Watu wakisimama karibu na nyumba zao mjini Juba, Februari 5, 2023, baada ya serikali kufunga shule zote kutokana na joto kali. Picha ya AP
Watu wakisimama karibu na nyumba zao mjini Juba, Februari 5, 2023, baada ya serikali kufunga shule zote kutokana na joto kali. Picha ya AP

Serikali ya Sudan Kusini Jumanne ilisema shule zitafunguliwa tena wiki ijayo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kutokana na joto kali nchini kote.

Wizara za afya na elimu zilisema viwango vya joto vinatarajiwa kushuka sana huku msimu wa mvua ukitarajiwa kuanza siku zijazo.

Sudan Kusini katika miaka ya karibuni ilikumbwa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa, huku joto kali, mafuriko na ukame vikiripotiwa katika misimu tofauti.

Wakati wa wimbi la joto wiki iliyopita, nchi ilirekodi viwango vya joto hadi nyuzi joto 45.

Taasisi za elimu ya juu ziliendelea kufungua milango.

Forum

XS
SM
MD
LG