Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 10:43

Mvua kubwa huko Dubai imesababisha mafuriko na uharibifu wa mali


Mvua kubwa iliyonyesha katika mitaa ya Dubai
Mvua kubwa iliyonyesha katika mitaa ya Dubai

Mvua ilianza usiku kucha na kuvuruga safari za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai

Mvua kubwa ilinyesha katika Umoja wa Falme za Kiarabu leo Jumanne na kusababisha mafuriko katika sehemu za barabara kuu na kuyaacha magari yakiwa yametelekezwa katika barabara kuu za Dubai.

Wakati huo huo idadi ya watu waliofariki katika mafuriko makubwa katika nchi jirani ya Oman imeongezeka na kufikia 18 huku wengine wakiwa bado hawajulikani walipo wakati taifa hilo la kisultani likijiandaa kwa kimbunga hicho.

Mvua ilianza usiku kucha na kujaza maji madimbwi makubwa mitaani huku upepo mkali ukivuruga safari za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, ambao una harakati nyingi sana duniani kwa safari za kimataifa na pia ni makaazi ya shirika la ndege ambalo linatoa huduma za masafa marefu la Emirates.

Polisi na wafanyakazi wa huduma za dharura walipita taratibu katika mitaa iliyofurika, taa zao za dharura zikiwaka asubuhi yenye giza. Radi nayo ilipiga na mara kwa mara ikigusa ncha ya Burj Khalifa, jengo refu zaidi duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG