Mohammed Fattah al-Burhan Rahmane alikuwa akiendesha pikipiki katika mji kuu wa Ankara, wakati alipogongana na gari kubwa siku ya Alhamisi na pikipiki yake kurushwa mita kadhaa, limeripoti shirika la habari la DHA.
Mtoto huyo wa jenerali wa Sudan alihamishwa hospitali ambako amelazwa katika chumba cha watu mahututi, ripoti hiyo iliongeza.
Ubalozi wa Sudani mjini Ankara hhaukujibu mara moja ulipoombwa kutoa maoni.
Tangu mwezi Aprili, Burhan amekuwa vitani na aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF).
Majenerali hao wawili walitofautiana baada ya mapinduzi ya kijeshi ya pamoja ya mwaka 2021 ambayo yalivuruga kipindi tete cha mpito wa kidemokrasia nchini Sudan.
Vita hivyo vimeua maelfu ya watu, ikiwa pamoja na 15,000 katika mji mmoja wa West Darfur, kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.
Pia umedhoofisha a uchumi, kuharibu miundo mbinu na kuwalazimisha zaidi ya watu milioni nane kukimbia makazi yao, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa