Takriban watu 37 walifariki katika jaribio hilo na 76 bado hawajulikani walipo.
Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu (Amnesty International) Ijumaa iliishutumu Morocco na Uhispania kwa kufanya njama za kuficha vitendo vya kibaguzi vya maafisa wao mpakani.
Kikundi hicho kimesema Uhispania ilishindwa kuanzisha uchunguzi huru baada ya waendesha mashtaka wa Uhispania kusitisha uchunguzi wao kwa sababu walisema hawakuons mwenendo wowote wa kihalifu uliofanywa na vikosi vya usalama vya Uhispania. Morocco haikufungua uchunguzi kabisa, kikundi hicho kilisema.
“Upande wa mpaka wa Morocco, na kufuatia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, mamlaka nchini Morocco ziliendelea kuwazuia Watu Weusi kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kuingia Uhispania ili waweze kuomba hifadhi ya ukimbizi katika ofisi za mpakani,” AI ilieleza katika taarifa yake.
“Kilichotokea huko Melilla ni ukumbusho kuwa sera za uhamiaji za kibaguzi zilizokusudia kufunga mipaka na kuzuia njia salama na za kisheria kwa watu wanaotafuta usalama huko Ulaya zina matokeo ya hakika na mabaya sana, Katibu Mkuu wa AI, Agnes Callamard alisema katika taarifa hiyo.
“Ni vigumu kuepuka uchochezi wa misimamo ya kibaguzi y akile kilichotokea Melilla na namna vitendo visivyo vya kibinadamu wanavyofanyiwa watu Weusi katika mipaka ya Ulaya, wanapoishi, wanapopotea au kufa.”
Taasisi hiyo ilisema miili 22 kutoka katika tukio hilo iko katika chumba cha maiti nchini Morocco.
Imetayarisha na mwandishi wa VOA Fern Robinson.