Utawala wa Biden umesema Jumanne utaongeza muda hadi mwaka 2025 wa kuwa na hadhi ya kisheria ya muda kwa wahamiaji zaidi ya 300,000 kutoka El Salvador, Honduras, Nepal na Nicaragua ambao walikabiliwa na hatari ya kufukuzwa na kupoteza vibali vya kazi chini ya sera za utawala wa Trump.
Chini ya mpango wa Hali ya Ulinzi wa Muda, utawala wa Biden utaruhusu wahamiaji kutoka nchi hizi nne kuendelea na makazi yao halali pamoja na ajira nchini Marekani.
Waziri wa Usalama wa Ndani, Alejandro Mayorkas alisema katika taarifa kwamba kupitia upanuzi wa Hali ya Ulinzi wa Muda-Temporary Protected Status, tuna uwezo wa kutoa usalama na ulinzi kwa walengwa wa sasa ambao ni raia wa El Salvador, Honduras, Nepal, na Nicaragua ambao tayari wapo Marekani na hawawezi kurudi kwa sababu ya athari za majanga ya kimazingira.
Program ya TPS haikupatii makazi ya kudumu nchini Marekani, lakini inatoa hadhi ya kisheria nchini Marekani na ulinzi wa kutofukuzwa kwa hadi miezi 18. Pia inatoa vibali vya kazi kwa watu kufanya kazi kisheria nchini. Na inaweza kuongezwa.
Forum