Misri: Sisi ashinda uchaguzi wa rais muhula wa tatu kwa asilimia 89.6

Abdel Fattah al- Sisi

Abdel Fattah al- Sisi ameiingia ameshinda kwa kishindo muhula wa tatu madarakani kama  rais wa  Misri kwa kipindi cha miaka sita asilimia 89.6 ya kura katika uchaguzi ambao hakupata changamoto kubwa, tume ya taifa imetangaza Jumatatu.

Uchaguzi umefanyika wakati Mirsi inataabika na mzozo wa kiuchumi na kujaribu kudhibiti kuingia hatari ya vita vya ukanda wa Gaza ambayo inapakana na peninsula ya Sinai huko Misri.

Baadhi ya wapiga kura wamesema kuzuka kwa mzozo wa Gaza kumewashawishi wao kumpigia kura sisi ambaye yeye mwenyewe ameonyesha kuwa thabiti katika eneol hilo tete , jambo ambali limethibitishwa kwa washirika wa ghuba na magharibi kutoa msaada wa kifedha katika serikali yake.

Uchaguzi huko Misri ulifanyika Desemba 10-12 huku serikali na vyombo vya habari vya ndani vinavyodhibitiwa vikali vikijitahidi kuongeza ushiriki ambao mamlaka za uchaguzi zilisema ulifikia asilimia 66.9 juu ya asilimia 41 zilizorekodiwa katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2018.

Uchaguzi huo uliwashirikisha wagombea wengine watatu hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na hadhi ya juu . mpinzani mashuhuri zaidi alisitisha ugombea wake mwezi Octoba akisema maafisa na majambazi wamelenga wafuasi wake shutuma ambazo zilitupiliwa mbali na tume ya taifa ya uchaguzi.

Chanzo cha habari hii ni mashirika mbalimbali ya habari.