Wafanyakazi wa uokoaji wamegundua miili 11 zaidi ya watu waliofariki katika mafuriko ya Jumanne usiku katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa.
Miili hiyo iligundulika katika wilaya ya kaskazini ya Mont-Ngafula mjini humo ambako nyumba nyingi zilizojengwa kwenye maeneo yenye vilima amayo yamekumbwa na maporomoko ya ardhi.
Mafuriko yameelezewa kuwa mabaya sana katika miaka kadhaa kusuhudiwa mjini humo.
Takriban nyumba 30,000 zimeathiriwa, huku nyumba 280 zikiwa zimeoshwa na maporomo ya ardhi.
Idadi rasmi ya vito ni 120 lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema zaidi ya watu 140 wamefariki.
Uharibifu kwa miundo mbinu ni mkubwa sana, huku wakazi wengi wa mjini humo wakikumbwa na uhaba mkubwa wa maji na kukatika kwa umeme.