Mdahalo huu ni fursa kwa wagombea wote wawili kujaribu kutengeneza tena maelezo ya kisiasa na kuwashawishi wapiga kura waliokuwa hawana uamuzi wampe nani kura zao.
Biden, mdemokratiki aliyeko madarakani, ana fursa ya kuwahakikishia wapiga kura tena kuwa, akiwa na umri wa miaka 81, anauwezo wa kuiongoza Marekani kukabiliana na changamoto kadhaa.
Wakati huohuo, Trump mwenye umri wa miaka 78 anaweza kutumia fursa hiyo kujaribu kuonyesha kukutwa na makosa ya uhalifu New York hakumshughulishi na kuwashawishi mamilioni ya watu kuwa anasifa za kuweza kurejea tena Ikulu kuongoza nchi.
Mdahalo wa Alhamisi huko Atlanta utaweka rikodi kwa kuongoza kwa mara ya kwanza – haikuwahi kutokea huko nyuma wagombea wawili wanao wania kuingia White House wakikabiliana katika umri mkubwa, na kabla ya hapo haijawahi kutokea CNN kuwa wenyeji wa mdahalo wa uchaguzi mkuu wa rais
Chanzo cha habari hii ni CNN