Waziri Mkuu Pravind Jugnauth amesema hatua hiyo huenda ikasaidia kuepusha misongamano, na kuongeza kuwa wanunuzi watapewa muda wa dakika 30 kununua bidhaa.
Hii ina maana kwamba wale ambao majina yao ya mwisho yanaanza na herufi A mpaka F watafanya manunuzi siku ya Jumatatu na Alhamisi na wenye majina ya wisho yanayo anzia G mpaka N watafanya manunuzi siku ya Jumanne na Ijumaa na wenye majina ya mwisho O mpaka Z watafanya manunuzi Jumatano na Jumamosi.
Maduka yatafungwa siku ya Jumapili.
Jumanne taifa hilo la kisiwani liliripoti kifo cha tano kufuatia mlipuko wa COVID-19 tangu kuripotiwa maambukizi nchini humo.
Muathirika wa karibuni alikuwa mwanamme mwenye umri wa miaka 71 ambaye alilazwa hospitali tangu Jumapili.
Mamlaka zinasema watu 161 wenye Covid-19 wanatibiwa katika mahospitali kote nchini humo.
Kiasi cha watu 1,709 wako katika karantini kwenye vituo maalum vya serikali na hoteli binafsi.
Waziri mkuu pia ametangaza kuongeza muda wa kuzuia watu kutosha nje mpaka Aprili 15.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC.