Wakati huohuo, Umoja wa Ulaya na India zimetangaza masharti makali ya kudhibiti usafiri kwenye mipaka.
Uingereza imepiga marufuku safari za ndege kutoka Afrika kusini na kuomba wasafiri raia wa Uingereza kukaa karantini wakirudi nyumbani kutoka huko. Naye mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya pia unalengo la kusitisha safari za ndege katika eneo lake.
Idara ya usalama wa afya ya Uingereza imesema aina hiyo mpya ya virusi ina protini kali ambayo ni tofauti kabisa na ile ambayo ilitumiwa kutengeneza chanjo ya COVID-19.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linafanya mkutano wa wataalamu wa afya leo kujadili aina hiyo mpya ya virusi vya corona na athari zake.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters