Mashoga wadai matumaini ni madogo kwa mahusiano yao kubarikiwa

Watuhumiwa wawili wanaodaiwa kijihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakiwa wamevaa sale ya gerezani ya rangi ya kijani wakiwa mahakamani Januari 22, 2014 PIcha na AFP

Watu wanaojihusisha na uhusiano wa jinsia moja wana matumaini madogo kwa makanisa yao kubariki mahusiano ya jinsia moja hivi karibuni, wakati wachungaji wa conservative kote barani Afrika wameamua kupuuza uamuzi wa kihsitoria wa Vatican kuruhusu baraka za aina hiyo.

Wanigeria Jane na Lucy ambao ni wapenzi na waumini wa kanisa Katoliki ambalo Wakatoliki waconservative wamelaani tangazo lililotolewa wiki mbili zilizopita, ambalo liliidhinishwa na Papa Francis, kuwa litaruhusu baraka kwa wapenzi ya jinsia moja, isipokuwa kama hawatakuwa sehemu ya watu wanaohudhuria ibada za kanisa.

Papa alijibu ukosoaji na kile alichokiita kuwa misimano ya kiitikadi isiyotaka kubadilika ambayo inalizuia kanisa kusonga mbele.

Lakini katika nchi nyingi za Afrika, kama vile Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambako mahusiano ya jinsia moja yamepigwa marufuku na mara nyingi adhabu yake ni kifungo kirefu jela.

Cha ajabu ni kwamba Jane mwenye umri wa miaka 39 amekuwa akiishi na mpenzi wake kwa muda wa miaka sita, hadhani kuwa tamko la Vatican litaleta mabadiliko.
“Labda katika kipindi cha miaka 20 au 30 ijayo, lakini kwa sasa ni vigumu kwa (maaskofu) kulikubali hili” Jane aliliambia Shirika la habari la Reuters ndani ya chumba chake huko katika jimbo la kaskazini kati la Benue.

Maaskofu wakatoliki wa Angola, Kenya, Nigeria, Malawi mpaka Sao Tome and Principe, Uganda and Zimbabwe ni miongoni mwa viongozi wa dini ambao wamesema hawatabariki watu wenye mahusiano ya jinsia moja, lakini wamesema kuwa amri ya Papa inaweza kutafsiriwa kama hiari. Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters