Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer na Seneta Mrepublikan Mike Crapo ni kati ya wale ambao watakuwa katika ziara hiyo.
Ofisi ya Schumer ilisema mwezi uliopita safari hiyo itajumuisha kusimama nchini Japan na Korea Kusini.
Ziara hii inakuja wakati maafisa wa Marekani wamekuwa wakiboresha mawasiliano na maafisa wa China, ikiwemo ziara kadhaa walizofanya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, Waziri wa Fedha Janet Yellen na Waziri wa Biashara Gina Riamondo huko China.
Kuongezea maelezo yao juu haja ya kuwepo njia za wazi za mawasiliano, maafisa wa Marekani pia wamegusia umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa masuala kama vile biashara, na changamoto ambazo biashara za Marekani zinazo endeshwa China zinakabiliana nazo.
Baadhi ya taarifa hii katika ripoti hii inatokana na shirika la habari la Reuters.