Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:02

Baraza la Wawakilishi la Marekani lapitisha mswaada wa sheria kuifadhili serikali kuu kwa siku 45


Jengo la Bunge la Marekani.
Jengo la Bunge la Marekani.

Baraza la wawakilishi la Marekani Jumamosi limepitisha mswaada wa sheria wa kuifadhili serikali kuu kwa siku 45 na hivvo kuepusha kufungwa kwa shughuli za serikali. Mswaada huo ulipitishwa kwa theluthi mbili ya Wabunge wote.

Mswaada huo ulipitishwa kwa kura 335 dhidi ya 91.

Muda wa matumizi ya fedha za serikali ulitarajiwa kumalizika leo Jumamosi Septemba 30 kabla ya usiku wa manane. Awali wabunge wa mrengo mkali wa kulia katika chama cha Republican walitishia kutoidhinisha mswaada wa kuifadhili serikali ikiwa serikali ya Rais Joe Biden haitapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yake hasa kwenye miradi ya lishe kwa watoto wa shule na familia zenye kipato cha chini, pia kusitisha mswaada wa dola bilioni 6 kwa Ukraine.

Mswaada huo unatakiwa kupitishwa na Baraza la Seneti na kusainiwa na Rais Joe Biden kuwa sheria.

Mamilioni ya wafanyakazi wa serikali kuu wakiwemo wanajeshi walikuwa katika hatari ya kutolipwa mishahara yao, maelfu ya wengine wangelazimika kufanya kazi bila malipo endapo shughuli za serikali zingefungwa.

Forum

XS
SM
MD
LG