Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:56

Dianne Feinstein, Seneta aliyetumikia kwa muda mrefu afariki akiwa na miaka 90


Hayati Dianne Feinstein
Hayati Dianne Feinstein

Dianne Feinstein, Seneta aliyetumikia kwa muda mrefu katika Baraza la Seneti la Marekani,  akiwakilisha Jimbo la California, afariki akiwa na umri wa miaka 90, chanzo cha habari kinacho fahamu taarifa hii kilisema Ijumaa. 

Seneta Feinstein, atakumbukwa kwa uhamasishaji wa udhibiti wa bunduki ambaye aliongoza katazo la kwanza la silaha za kivita la serikali kuu na kusajili utesaji uliofanywa na CIA kwa washukiwa wa ugaidi wa kigeni.

Ofisi ya Feinstein haikutoa majibu mara moja kuhusu ombi la maelezo ya habari za kifo chake, zilizo kuwa awali zimeripotiwa na shirika la habari la Punchbowl.

Feinstein alikuwa ni mfano kwa Washington ambaye pamoja na mafanikio mengine alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Kamati ya Usalama ya Seneti yenye ushawishi mkubwa.

Katika kipindi cha miaka 31 katika Seneti alikuwa amejipatia umaarufu wa kuwa mliberali mwenye msimamo wa kati, wakati mwengine akichukiwa na wale wa mrengo wa kushoto.

Feinstein alijiunga na Seneti mwaka 1992 baada ya kushinda uchaguzi maalum na alichaguliwa katika mihula mitano ikiwa pamoja na mwaka 2018, na hivyo kuwa seneta mwanamke aliyetumikia kwa kipindi kirefu zaidi kuliko mwengine yoyote.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG