Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:39

Rais Biden asema Trump ni tishio kwa demokrasia


Rais wa Marekani, Joe Biden, amezidisha mashambulizi yake dhidi ya rais wa zamani Donald Trump, Alhamisi, katika hotuba kali ambayo amewahi kutoa hadi sasa, kwamba rais huyo wa zamani na mgombea anaeongoza katika chama cha Republikan, ni kitishio kwa desturi na taasisi za kidemokrasia za nchi.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika jimbo la magharibi la Arizona, rais Biden, amemshutumu Trump kwa kuwa na dhana za hatari kwa kuona kuwa na nguvu isiyosimamiwa na yupo juu ya sheria.

Amemnukuu rais mstafu Trump kuwa anasema katiba inampa haki ya kufanya chochote anachotaka kama rais.

Rais Biden amesema hajawahi kusikia rais akiwa anasema hivyo. Mwaka 2019, Trump alisema kwamba ana haki hiyo chini ya ibara ya pili ya katiba ambayo inazungumzia madaraka ya rais.

Mwezi Machi aliwaeleza wafuasi wake kwamba yeye ni haki yao, na wote ambao wamekuwa wakifanyiwa mabaya yeye ndiye mtetezi wao.

Forum

XS
SM
MD
LG