Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:59

Baraza la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na Warepublikan litafanya kikao cha uchunguzi kumshtaki Rais Biden


Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na mtoto wake Hunter Biden (kushoto)
Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na mtoto wake Hunter Biden (kushoto)

Hatua hii inajiri siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho kwa Bunge la Marekani kuzuia serikali kuu kufungwa.

Usikilizaji unaofanywa na Kamati ya Uangalizi katika Bunge hauonekani utabaini habari mpya juu uhusiano wa kifedha wa Biden kwa mtoto wake Hunter Biden.

Mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 53 ambaye alikumbwa na misukosuko, na pia aliingia ubia katika makampuni mbalimbali ya kimataifa, huku akipambana na matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

Badala yake usikilizaji huo utatumika kama uhalalishaji wa aina ya uchunguzi na tathmini ya kile maelezo ya Warepublican waliyoyapata hadi sasa, hiyo ni kulingana na James Comer mwenyekiti wa jopo.

Wabunge watasikiliza maelezo kutoka kwa mhasibu wa uchunguzi, afisa wa zamani wa wizara ya sheria ya Marekani na profesa wa sheria.

Forum

XS
SM
MD
LG