Marekani yazitaka nchi za Ghuba kuongeza usambazaji mafuta kujazia upungufu wa mafuta ya Russia

FILE PHOTO: Mabomba ya mafuta ghafi wakati wizara ya Nishati ilipotembelea Kituo cha Mafuta cha Kimkakati huko Freeport, Texas, Marekani Juni 9, 2016. REUTERS/Richard Carson/File Photo

Marekani imepiga marufuku uagizaji wa nishati ya Russia na inaitaka Saudi Arabia kuongeza uzalishaji mafuta ili kupunguza ongezeko kubwa la bei ya mafuta. Haiko bayana kama mataifa ya Ghuba yako tayari kusaidia kushusha bei za mafuta.

Mivutano na Russia baada ya uvamizi wake nchini Ukraine ukiwa unaendelea na kusababisha kelele kwenye masoko ya ulimwengu, ikiwaadhibu wenye magari na wengine ambao wanaendelea kutegemea mafuta kwa siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani Joe Bden kupiga marufuku uagizaj wa mafuta, gesi na makaa ya mawe kutoka Russia.

Rais wa Marekani Joe Biden (AP Photo/Patrick Semansky, File)

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson pia amepiga marufuku uagizaji mafuta kutoka Russia ifikapo mwisho wa mwaka 2022.

Umoja wa Ulaya unaitegemea Russia kwa kiasi cha 40% ya gesi yake ya asili na kiasi cha 25% ya mafuta kwa ajili ya wateja wake. Viongozi 27 wa EU wamekubaliana kwa tahadhari “kujiondoa pole pole” katika utegemezi wao kwa nishati ya Russia.

Rais wa Russia Vladimir Putin aliilaumu Marekani na Ulaya kwa kupanda kwa bei za mafuta na gesi, na kusema hivi sasa wana haha kuwafikia wazalishaji wakubwa ambao awali waliwawekea vikwazo.

Rais wa Russia Vladimir Putin anasema “sasa wanajaribu kwa gharama zote kufikia makubaliano na nchi ambazo ziko tayari kufikia amani na Iran na haraka kutia saini nyaraka zote. Pamoja na Venezuela.”

Huku bei za mafuta zikiwa zimepanda sana kwenye vituo vya kuuzia mafuta, Rais Biden anasema amewasiliana na Saudi Arabia, lakini Prince Mohammed bin Salman hajachukua simu yake.

Biden alizungumza na mfalme wa Saudia Salman hapo Februari 9.

Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud (Picha na Biro Setpres RI)

Uhusiano kati ya Marekani na mwana mfalme umekuwa wa mivutano tangu mauaji ya kikatili na kukatwakatwa kwa mwana habari wa Washington Post Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mwaka 2018.

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alitoa uzito mdogo wa Saudia ‘kutopokea’ simu ya Biden na kusema kuna habari za kutia moyo kuhusu uzalishaji mafuta kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu.

“Kulikuwa na tangazo muda mchache uliopita, sina uhakika kama limetolewa hadharani, kuhusu uungaji mkono wa Emirati kuongeza uzalishaji wakati inapokuwa ni OPEC, ambapo nadhani ni jambo muhimu kuleta uthabiti wa masoko ya nishati ulimwenguni, kuhakikisha kwamba kuna kiwango kikubwa cha nishati kote duniani.

Watalaamu wameiambia VOA kuna mivutano kati ya Biden na mwana mfalme wa Saudi Arabia, lakini maafisa wa utawala wa Biden wamekuwa wakifanya mazungumzo huko Riyadh.

“Nadhani wasi wasi mkubwa ni kwamba wakati ambapo bei za mafuta zimepanda sana, tunaangalia kupata ushirikiano fulani kutoka nchi nyingine, zikiwemo wale washirika wa karibu ambao wananufaika na ushirikiano wetu wa kiusalama na misaada, tuna matumaini kwamba huenda watafanya mengi zaidi kuisaidia Marekani.”

Brian Katulis wa Taasisi ya Mashariki ya Kati anasema kuna hatari fulani kwa Saudi Arabia kama ikikataa kushusha bei za mafuta.

“Kuna matatizo ya kisiasa hapa, kutoka kwa wote Warepublican na Wademocrat, kama wateja ambao ni wenye magari hawataki kulipa bei kubwa ya mafuta, watamuangalia mtu wa kumlaumu. Nadhani nchi kama Saudi Arabia, imekuwa ikilaumiwa hapo kabla kwasababu ya marufuku ya OPEC mwishoni katika miaka 1970, huenda ikawa rahisi kupata wa kumlaumu.”

Maafisa wa Utawala wa Biden pia wamefanya mazungumzo na nchi yenye utajiri wa mafuta Venezuela mwezi huu na wana matumaini ya kufikia makubaliano katika mazungumzo ya nyuklia na Iran huko Vienna, ambayo hatimaye huenda yakaachia mafuta ya Iran kurejea kwenye soko la ulimwengu. Lakini mazungumzo yamesitishwa kutokana na madai mapya ya Russia kwa masharti yasiyokuwa na vikwazo vya biashara na Iran.