Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:42

Washington inaionya Moscow kuhusu uvamizi wake kwa Ukraine


Rais wa Russia, Vladmir Putin
Rais wa Russia, Vladmir Putin

Washington siku ya Alhamis iliionya Moscow kuhusu kile ambacho baadhi ya waangalizi wanakielezea kama uhalifu wa kivita unaofanywa na vikosi vya Russia nchini Ukraine.

Maafisa wa marekani wanasema Russia “inageukia mkakati wa kuweka taka kwenye vituo vya idadi ya watu nchini Ukraine” huku mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya pande zinazozozana hayajafanikiwa. Tumeona ripoti za kuaminika za mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia ambayo chini ya mikataba ya Geneva yangekuwa uhalifu wa kivita, alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marekani, Ned Price japokuwa hakuishutumu kabisa Russia kwa kufanya uhalifu kama huo.

Mpango wa Rais wa Russia, Vladmir Putin wa kuikamata Ukraine haraka ni wazi sasa umeshindwa Price alisema kuhusu uvamizi huo wa wiki mbili. Kwa hivyo sasa anageukia mkakati wa kuweka taka kwenye vituo vya watu ili kujaribu kuvunja matakwa ya watu wa Ukraine jambo ambalo hawataweza kulifanya.

Russia imekanusha kuwalenga raia katika uvamizi wake nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG