Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:36

Zelensky aitaka EU kuisaidia Ukraine zaidi


Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky akiwa katika mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani Joe Biden. Picha na shirika la habari la Reuters
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky akiwa katika mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani Joe Biden. Picha na shirika la habari la Reuters

Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amesema Ijumaa Umoja wa Ulaya unapaswa kufanya zaidi kwa nchi yake iliyokumbwa na mzozo, siku moja baada ya viongozi wa umoja huo kuonyesha matumaini ya nchi yake kuingia haraka katika umoja huo.

Alitoa maelezo hayo baada ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, kusema kuwa watu milioni 2.5 sasa wamekimbia Ukraine huku sita kati ya 10 wakiwa katika nchi jirani ya Poland, upande wa Magharibi.

UN ilikuwa inajipanga kwa ajili ya watu milioni nne kukimbia katika nchi hiyo kufuatia uvamizi wa kijeshi Russia ulioanza Februari 24.

Mjini Moscow Rais wa Russia Vladmir Putin alisema kulikuwa na mabadiliko chanya ya mazungumzo baina ya Russia na Ukraine, ikiwa ni wiki mbili za kampeni za kijeshi za Moscow nchini.

“ kuna mabadiliko chanya, wapatanishi kutoka upande wetu waliripoti kwangu,” Putin alimwambia mwenzake wa Belarus Alexander Lukashenko wakati wa mkutano uliotangazwa kwenye televisheni mjini Moscow.

Aliongeza kusema kuwa mazungumzo sasa yanafanyika karibu kila siku. Wapatanishi wa Russia na Ukraine wamefanya duru kadhaa za mazungumzo tangu Putin alipotuma majeshi yake nchini Ukraine February 24.

Naye Mkuu wa NATO Jens Stolten-berg alisema leo kwamba NATO isiruhusu uvamizi wa Russia huko Ukraine kuvuka na kuwa mzozo baina ya washirika na Moscow.

XS
SM
MD
LG