Mahakama ya juu kuamua leo iwapo Trump aondolewe katika uchaguzi 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anaweza kujua leo ikiwa Mahakama ya Juu itamruhusu kushiriki katika uchaguzi mwaka 2024, wakati ambapo mgombea huyo mkuu wa chama cha Republican akiwa anakaribia katika uteuzi wa chama chake.

Majaji wanatarajiwa kuamua angalau kesi moja Jumatatu kukiwa na ishara kwamba uamuzi wa kesi hiyo huko Colorado ambayo inatishia kumfuta Trump katika baadhi ya vituo vya kura za majimbo kwa sababu ya juhudi zake za kubatilisha uchaguzi 2020.

Trump anapinga uamuzi wa msingi wa Mahakama ya juu ya Colorado ambayo ilisema kuwa ameondolewa kwenye nafasi ya kuwania tena urais na hastahili kuwepo katika uchaguzi wa mchujo wa jimbo hilo ambao ni kesho jumanne.

Maamuzi ya kesi hiyo leo , siku moja kabla ya kinyang’anyiro cha Super Tuesday kwenye majimbo 16 litaondoa sintofahamu kuhusu iwapo kura za Trump zitahesabiwa.

Pande zote mbili zimieomba mahakama ifanye haraka ambapo ilisikiliza majadiliano chini ya mwezi mmoja uliopita , Februari 8.