Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 23:21

Ombi la Trump la kutaka asilipi faini ya dola milioni 454 lakataliwa na Jaji


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akihudhuria kesi ya ulaghai dhidi yake katika mahakama kuu ya serikali mjini New York, Januari 11, 2024.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akihudhuria kesi ya ulaghai dhidi yake katika mahakama kuu ya serikali mjini New York, Januari 11, 2024.

Jaji wa mahakama ya rufaa ya New York, Jumatano alikataa ombi la Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kusitisha tozo ya faini ya dola milioni 454 katika kesi ya ulaghai dhidi yake, na kupinga ombi la mwanasiasa huyo kutaka aruhusiwe kutoa dhamana ya kiwango kidogo cha pesa anazodaiwa.

Jaji Anil Singh aliamuru Trump kutoa dhamana ya kiwango chote cha faini hiyo ili kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo.

Jaji Singh alikubali baadhi ya maombi ya Trump, ikiwemo kusitisha marufuku ya miaka mitatu ya kuomba mikopo kwenye benki za New York, hatua ambayo inaweza kumsaidia kupata dhamana inayohitajika.

Mawakili wa Trump mapema Jumatano waliiambia mahakama ya rufaa kwamba Trump yuko tayari kutoa dhamana ya dola milioni 100, wakieleza kuwa marufuku ya kuomba mikopo katika uamuzi wa Februari 16 ilifanya iwe kikwazo kwake kupata dhamana ya kiwango chote cha dola milioni 454.

Forum

XS
SM
MD
LG