Mahakama ya Juu India yakubaliana na hatua ya serikali kufuta uhuru kiasi wa eneo la Kashmir

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Mahakama ya Juu nchini India Jumaztatu imekubaliana na hatua ya serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi kufuta uhuru kiasi wa eneo la Kashmir ambalo lina Waislam waliowengi, ambako uasi ulikuwa unaendelea kwa miongo kadhaa, na kuamuru uchaguzi ufanyike ndani ya mwaka mmoja.

Azimio la 2019 lilikuwa “kukamilika kwa mchakato wa kuiunganisha nchi na hasa hatua ya kutumia madaraka yaliyo halali”, Mahakama ya Juu ilisema katika uamuzi wake.

Hatua hiyo iliambatana na kuwekwa kwa utawala wa moja kwa moja kutoka New Delhi, kukamatwa watu kwa jumla, amri ya kutotoka nje na kufungwa kwa mawasiliano kulikoendelea kwa miezi kadhaa wakati India ikiimarisha uwepo wa majeshi yake katika mkoa huo ili kudhibiti maandamano.

Sera ya mabavu ya Modi imekuwa yenye utata mkubwa huko Kashmir lakini ilisherehekewa na wengi kote India, wakati uasi ambao uligharimu maisha ya maelfu ya watu kwa miongo kadhaa kuzimwa kwa kiwango kikubwa.

Askari wa miamvuli wakilinda doria katika mji wa Srinagar Desemba 11, 2023. (Photo by TAUSEEF MUSTAFA / AFP)

Kuondolewa kwa Kifungu cha 70 cha katiba, kilicho toa hadhi maalum kwa eneo hilo la utawala la India, imepingwa na vyama vya siasa vyenye kuiunga mkono Kashmir, Jumuiya ya Mawakili wa eneo na wanasheria mbalimbali, kutokana na uamuzi wa mahakama Jumatatu.

Mahakama hiyo ilikubaliana na kuondolewa kwa uhuru wa mkoa huo na kutaka Jammu na Kashmir, kama ilivyojulikana ziko chini ya utawala wa Delhi, zirejeshwe kuwa jimbo na kuwa sawa na majimbo mengine ya India “haraka iwezekanavyo na mara moja.”

Mahakama hiyo pia imeagiza uchaguzi wa jimbo ufanyike ifikapo Septemba 30, 2024.

Ulinzi uliongezwa kote katika eneo linalotawaliwa na India huko Kashmir kabla ya uamuzi huo wa mahakama, huku mamlaka zikipeleka mamia ya wanajeshi, askari wa miamvuli na maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Srinagar kuzuia maandamano.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.