India haitambui serikali ya Taliban ambayo ilichukua mamlaka mnamo 2021 na ilikuwa imemruhusu Balozi Farid Mamundzay na wafanyikazi wa Ubalozi kusalia, kutoa visa na kushughulikia maswala ya biashara.
Ubalozi huo ulisimamisha shughuli zake mwezi Septemba wakati balozi na wafanyakazi wakuu walipoondoka kuelekea Ulaya na Marekani kutafuta hifadhi.
Siku ya Ijumaa, ubalozi huo ulichapisha taarifa kwa mtandao wa X, ikisema kuwa ubalozi huo ulikuwa umefungwa na kwamba funguo kukabidhiwa serikali ya India. Aidha ubalozi wa Afghanistan ulisema shinikizo kutoka kwa serikali ya India na Taliban zililazimisha uamuzi huo.
Forum