Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:25

IMF yasema Malawi inahitaji dola bilioni 1 kushughulikia madeni yake


Malawi inahitaji karibu dola bilioni 1 ili kufanya marekebisho ya malipo au kusamehewa madeni yake kutoka kwa wakopeshaji wake ifikapo mwaka 2027, shirika la kimataifa la fedha limesema Jumatano, wakati ikipambana na uhaba mkubwa wa dawa, mafuta na mbolea kutokana na uhaba wa fedha za kigeni.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika isiyo na bandari inahitaji dola milioni 887 ili kurekebishiwa madeni kutoka 2023 hadi 2027 kutoka kwa wakopeshaji wake wa kibiashara na dola milioni 99 kutoka kwa wakopeshaji wake wa IMF imesema katika ripoti.

Bodi ya utendaji ya IMF iliidhinisha mkopo wa dola milioni 178, wa miaka minne kwa Malawi wiki iliyopita.

Kupata ahadi kutoka kwa wadai wake mataifa mawili ya China, na India, kurekebisha sehemu yao ya madeni yake ya nje, ambayo ilikuwa ni dola bilioni 4 mwishoni mwa 2022, lilikuwa hitaji kuu kwa bodi ya IMF ili kuidhinisha mkopo huo.

Forum

XS
SM
MD
LG