Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 06:02

Kimbunga chasababisha maelfu ya watu India kuyahama makazi yao


Wafanyakazi wa Kikosi cha Taifa cha Kukabiliana na Majanga (NDRF) wakati wa operesheni ya uokoaji huko Chennai Desemba 4, 2023. Picha na R. Satish BABU / AFP.
Wafanyakazi wa Kikosi cha Taifa cha Kukabiliana na Majanga (NDRF) wakati wa operesheni ya uokoaji huko Chennai Desemba 4, 2023. Picha na R. Satish BABU / AFP.

Mitaa ya Chennai imefurika baada ya mvua kubwa kunyesha kusini mwa India huku mamlaka ikilazimika kufunga shule na ofisi, kusimamisha safari za ndege na kuwahamisha watu wanaoishi maeneo ya pwani kabla ya dhoruba kali inayotarajiwa kuanza katika saa 24 zijazo.

Mamlaka ya Kitamil Nadu na jirani Andhra Pradesh walitoa tahadhari kubwa, mamlaka katika majimbo yote mawili yakionya wavuvi dhidi ya kujitosa baharini kwa uvuvi.

Uwanja wa ndege wa Chennai ulisimamisha shughuli zake kwa saa mbili Jumatatu asubuhi baada ya mvua kubwa kunyesha jijini, ripoti za vyombo vya habari zilisema, na safari kadhaa za ndege zilikatishwa au kuelekezwa katika miji mingine.

Kimbunga Michaung kinatarajiwa kutua kwenye ufukwe wa Andhra Pradesh siku ya Jumanne asubuhi, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa nchini huku kukiwa na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilomita 110 kwa saa.

Forum

XS
SM
MD
LG