Jacob Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahakama baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa.
Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahakama baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa. Katika mwezi huo huo mahakama kuu ya Afrika kusini ilitupilia mbali ombi lake la kutengua hukumu hiyo.
Michakato ya kisheria dhidi ya Zuma kwa madai ya rushwa wakati wa utawala wake wa miaka tisa inatazamwa na wengi kama mtihani wa uwezo wa Afrika kusini baada ya enzi ya ubaguzi kuhusu uwezo wake kuimarisha utawala wa sheria hasa dhidi ya watu wenye madaraka na wenye uhusiano na uongozi.
Zuma alikwenda mwenyewe hapo Julai 7 kuanza kifungo chake na kusababisha ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Afrika kusini katika kipindi cha miaka kadhaa huku wafuasi wa Zuma waliokuwa na hasira wakiingia mitaani.