Kiongozi huyo alitoa hotuba hiyo kufuatia malalamiko, maandamano na ghasia za siku kumi kupinga kodi mpya ya mafuta ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Rais amefafanua kuwa : "Ndio ni lazima tusikilize kilio cha jamii yetu, lakini haijatulazimu kuchukua hatua kupinga wajibu wetu wa leo na kesho, kwa sababu kuna kilio kikubwa cha mazingira. Ninaweza hata kuongeza kwamba ni ukosefu wa usawa wa kijamii ambao wananchi wengi wanalaani hii leo.
Hata hivyo Rais Macron amelaani ghasia zilizotokea Ufaransa na majimbo yake yaliyoko n’gambo wakati wa maandamano hayo.
Ingawa amechukuwa msimamo huo mkali, kiongozi huyo katika kuwaridhisha waandamanaji amesema kutakuwa na marekebisho ya kodi hizo za mafuta kwa kutilia maanani ongezeko la bei ya mafuta duniani ili isiwe sababu ya kuwaadhibu wateja.
Kabla ya hotuba hiyo Rais Macron alikutana na baraza lake la mawaziri na waatalamu wa mazingira ili kuunda baraza kuu la hali ya hewa linalowaleta pamoja waatalamu wa mazingira.