Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:46

Trump : Marekani haitosaini makubaliano ya mkutano wa G-7

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na viongozi wa G7 Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe na Rais wa Marekani Donald Trump wakijadiliana juu ya makubaliano ya pamoja, Jumamosi, Juni 9, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumamosi kuwa alikuwa amewaamrisha wawakilishi wake wasisaini makubaliano yaliyofikiwa na viongozi saba wa mataifa ya G 7 yenye uchumi mkubwa duniani nchini Canada, akinukuu matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau baada ya kuondoka.

"Ni uwongo kabisa na dhaifu," Trump alituma ujumbe wa tweet kujibu maoni ya Trudeau kwamba ushuru mpya wa Marekani katika chuma na aluminum ilikuwa ni "makosa."

"Kutokana na kauli ya uongo ya Justin wakati wa mkutano na waandishi wa habari, na ukweli wa kuwa Canada inatoza ushuru mkubwa kwa wakulima, wafanyakazi na makampuni ya Marekani, nimewaamrisha wa wakilishi wetu kutosaini makubaliano hayo wakat tukiangalia ushuru unaotozwa kwa magari ambayo yanamiminika katika soko la Marekani!" Trump ameongeza.

"Uhusiano wa kimataifa hauwezi kulazimishwa kwa kutumia hasira kutoa tu maneno ovyo," Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imesema katika tamko lake juu ya kujitoa kwa Trump kusaini makubaliano hayo.

XS
SM
MD
LG