Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:09

Mwanamziki maarufu wa Ufaransa aaga dunia


FILE - French singer Charles Aznavour performs during the Quebec Summer Festival, July 6, 2008.
FILE - French singer Charles Aznavour performs during the Quebec Summer Festival, July 6, 2008.

Mwanamziki maarufu nchini Ufaransa Charles Aznavour – aliyesema wiki jana kwamba alitaka afe akiwa kwenye jukwaa akitumbuiza wafuasi wake, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 94.

Msemaji wake ameambia shirika la habai la AFP kwamba Aznavour, ambaye amerejea nyumbani kutoka kwa ziara ya kimziki nchini Japan, ameaga dunia akiwa nyumbani kwake, Alpilles, kusini mashariki mwa Ufaransa.

Mtumbuizaji wa siku nyingi nchini Ufaransa Alain Delon, amesema kwamba rafiki wake ameaga dunia akiwa usingizini.

Rais wa ufaransa Emmanuela Macron ameongoza taifa katika kuomboleza gwiji huyo wa muziki akimtaja kama mtu aliyekuwa na kipawa cha kipekee, huku waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan akimtaja kuwa shujaa wa taifa.

XS
SM
MD
LG