Vifo hiyo vilihusisha waandamanaji waliokuwa wameweka kambi nje ya makao makuu ya Wizara ya Ulinzi wakati wa kuwatawanya waandamanaji hao mwanzoni mwa mwezi wa Juni.
Msemaji wa baraza la mpito la kijeshi alieleza kuwa makundi mawili yanayo shukiwa kuhusika na majaribio ya mapinduzi walikamatwa.
Aliongeza kuwa kundi moja lilijumuisha watu watano wakati kundi jingine lilikuwa na zaidi ya watu 12.
Baraza la kijeshi lilifanya mapinduzi yaliyotokea April 11, wakati maafisa wa jeshi walipomuondoa madarakani na kumkamata rais wa zamani wa Sudan Omar al Bashir.
Mapinduzi hayo yalifuatia maandamano ya miezi kadhaa dhidi ya utawala wake wa miaka 30.
Uwanja nje ya wizara ya ulinzi mjini Khartoum, umekuwa kituo cha maandamano mapya wakati waandamanaji wakitoa wito kwa jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.