Your browser doesn’t support HTML5
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliongoza sherehe za kuadhimisha miaka 43 ya uhuru wan chi kutoka wa Uingereza, akiwasihi raia kuendelea kuungana wakati uchumi unafufuka. Aliongezea kwamba serikali imetekeleza “miradi mikuwa ya kubadili maisha” ili kuwainua wazimbabwe kutoka kwenye umaskini na kuingia katika ustawi.
“Inatia moyo kwamba mashinikizo ya mfumuko wa bei yanaendelea kupungua kutokana na mchanganyiko wa mikakati ya kifedha na sera kali za fedha. Upanuzi ukionekana wazi, uzalishaji na faidha zikionekana katika sekta zote za uchumi wetu ambao nchi unaziona zikiwa na kiwango cha juu cha wastani wa pato la ndani la jumla likiongezeka katika eneo letu,” anasema Mnangagwa.
Lakini kilometa chache kutoka hapo Florence Makashe, anauza viazi vitamu ili kuihudumia familia yake. Anasema serikali ya Mnangagwa ichukue hatua.
Makashe anasema “tumesuluhisha kwamba bei za bidhaa katika maduka yetu ni vyema zipunguzwe. Ada za shule zinaendelea kupanda. Tunapata simu kutoka shule zikitueleza kuhusu kupanda kwa ada. Hayo ni masuala makuu ambayo tunayalilia.”
Ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa April mwaka huu ilisema viwango vya umaskini bado viko juu ingawaje vinashuka.
John Maketo mkuu wa program katika Zimbabwe Coalition on Debt and Development, shirika lisilo la kiserikali linalounga mkono haki ya kijamii na kiuchumi, anasema sera potofu zinazopendelea wasomi ndiyo za kulaumiwa kwa kuendelea kwa umaskini.
“Unapokuwa na hali kama hii ambako sera haziangalii zaidi watu, matokeo yake ni kwamba unakuwa na idadi kubwa ya watu ambao wamegubikwa na umaskini,” anasema Maketo.
Aliongezea kwamba kwasababu ya deni kubwa sana la umma la Zimbabwe, nchi inashindwa kupata mikopo mipya, na matokeo yake ni uwekezaji mdogo katika ajira ili kupunguza umaskini. Hiyo imewaathiri watu kama Florence Makashe, ambaye anaishi katika umaskini.