Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:42

Zimbabwe yaonyesha mfano Afrika kwa kuidhinisha matumizi ya sindano ya kuzuia maambukizi ya HIV


Cabenuva (cabotegravir, rilpivirine) mwanzoni ilikuwa ni vidonge na vilikuwa vinamezwa kila siku.
Cabenuva (cabotegravir, rilpivirine) mwanzoni ilikuwa ni vidonge na vilikuwa vinamezwa kila siku.

Mwezi Oktoba, Zimbabwe imekuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kuidhinisha matumizi ya dawa kwa njia ya sindano ili kuzuia maambukizi ya HIV, dawa hiyo inaitwa Cabotegravir.

Mwandishi wetu wa Harare Columbus Mavhunga anaripoti kuwa wengi wana hamu kubwa ya kupatiwa dawa hii.

Mwanamke aeleza faida za kutumia sindano kuzuia HIV
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00

Mwanamke wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 32, ambaye aliomba kutotajwa jina lake, anasema alipigwa sindano ya kuzuia HIV inayoitwa Kaba-the-graveer wakati alipokuwa anafanya kazi nchini Marekani

Amekuwa akitumia dawa za HIV kila siku kwa miaka saba. Lakini baada ya kupigwa sindano hiyo mwezi Aprili na hivi kwa vile Zimbabwe imeidhinisha, ana matumaini ya kupigwa sindano hiyo kila miezi miwili.

Raia wa Zimbabwe Mtumiaji Cabotegravir anaeleza uzoefu wake: “Napendelea kupigwa sindano badala ya kutumia kidonge kwasababu sindano ni bora zaidi; unapigwa kila baada ya miezi miwili, kinyume na kidonge unatakiwa umeze kila siku wakati huo huo na kuna hatari ya kusahau kula kwasababu una mambo mengi ambayo yanaweza kutokea kwa siku katika maisha ya mtu. Kwa kweli, pengine utakwenda kwenye mazishi na kusahau kula dawa. Lakini kwa sindano unapigwa kila miezi miwili na ni sindano sita kwa mwaka, ambapo ni bora kuliko vidonge.”

Zimbabwe ni nchi ya kwanza kuidhinisha matumizi ya Kaba-the-graveer au CAB-LA. Marekan iliidhinisha dawa hiyo Desemba mwaka 2021 na Australia mwaka 2022.

Zimbabwe ilipitisha ushuru wa asimilia 3 kwa ajili ya Ukimwi mwaka 1999 ili kuisaidia nchi kujibu na kushughulikia masuala ya HIV and Ukimwi. Watu binafsi wanalipa kodi ya mapato ya asilimia 3 na waajjiri wanalipa asilimia 3 ya faida kwa juhudi hizo.

Shirika la Afya Duniani limeipongeza Zimbabwe kwa kuidhinisha dawa inayotolewa kwa njia ya sindano, ikisema itafungua njia kwa kuwapatia usalama zaidi na njia muafaka za kuzuia HIV.

Mamlaka ya udhibiti dawa ya Zimbabwe au MCAZ, inasema kwa sasa dawa hii imeruhusiwa tu kwa ajili ya kuzuia HIV.

Farai Masekela, Mamlaka ya Udhibi Dawa, Zimbabwe anaeleza: “Kutakuwepo na matayarisho mengine kuhusiana na cabotegravir, ambayo huenda yakawasilishwa baadaye na waombaji au watengenezaji wa dawa ambayo itatumiwa kwa ajili ya matibabu. Lakini hii ya sasa, ambayo imeidhinisha, ina maana ya kuzuia tu HIV, na siyo kwa matibabu.”

Dr. Nyaradzo Mgodi wa chuo Kikuu cha Zimbabwe cha utafiti wa majaribio ya kiafya katika nchi tisa za kiafrika, anasema dawa hii inafanya kazi vizuri na inataka Zimbabwe kuitoa kwa wote haraka iwezekanavyo.

Dkt Nyaradzo Mgodi, Chuo Kikuu cha Zimbabwe anasema: “Kwasababu kama wanawake wa kiafrika, tunaendelea kupata HIV kwa viwango vya kutisha na hata mmoja akipata maambukizi hayo ni mengi. Kama tuna kitu ambacho kinafanya kazi, lazima tuhakikisha kila mtu anakipata ambaye anakihitaji.”

Wafuasi wanasema upatikanaji wa dawa hiyo utawasaidia wazimbabwe kacha kutegemea nchi nyingine kupata dawa za kutibu HIV na Ukimwi.

XS
SM
MD
LG