Pamoja na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kukana mashtaka wiki iliyopita kwa jinsi alivyoshughulikia nyaraka za siri, kushtakiwa kwake hivi karibuni kunaendelea kuchochea mijadala mikali miongoni mwa wanachama wa chama chake.
Mgombea urais wa Republican and mwendesha mashtaka wa zamani, Asa Hutchinson amekiambia kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week” kwamba Trump ni vyema ajitoe katika kinyang’anyiro cha kuwania urais.
Asa Hutchinson, mgombea urais wa Republican anasema “KIla unapopata changamoto kadhaa za chunguzi tofauti wakati wa kipindi cha kuelekea mwaka ujao si haki kwa nchi, na kwa hakika si haki kwa chama ambacho kinataka nchi irejee kwenye mwelekeo wake.”
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha NBC, makamu rais wa zamani wa Marekani, Mike Pence, ambaye pia anawania urais, alihoji kwanini washindani wake katika uchaguzi wa awali wa Republican wanahisi kuwa Trump atakutwa na hatia.
“Angalia, tunachofahamu ni kile ambacho rais ameshutumiwa katika mashtaka yake. Hatufahamu ana utetezi gani. Hatuafahamu kama kesi itaendelea. Huenda likawa ni suala la kuwasilisha hoja kufutwa,” anasema Mike Pence.
Akiwa kwenye kituo cha televisheni cha CNN, mwenyekiti wa Kamati ya Upelelezi ya Bunge, Mrepublican Mike Turner, alisisitiza umuhimu wa kuuachia mchakato wa kisheria usonge mbele.
“Nina uhakika sitatetea tabia amayo imeorodheshwa kwenye malalamiko, lakini watathibitisha hilo,” Turner ameelezea zaidi.
Rais Joe Biden, ambaye alianza kampeni yake mwishoni mwa wiki kutaka kuchaguliwa tena amekataa kutoa maoni yake kuhusu changamoto za kisheria za Trump. Biden anaheshimu taratibu ambazo zinalinda uchunguzi.
Alielezea Seneta Mdemocrat Sheldon Whitehouse kwenye kituo cha televisheni cha ABC.
Seneta Sheldon anasema, “Hafanyi biashara na Mwanasheria Mkuu Garland. Hazungumzi naye kuhusu masuala yanayohusiu uhaifu. Na pili, Garland amekingwa na kushtakiwa kwasababu amemteua mwanasheria maalum. Uwezo wake wa kumhusisha mwanahseria mkuu una kikomo.”
Rais Biden mwenyewe anachunguzwa kwa shutuma za kushughulikia vibaya nyaraka za siri. Lakini hata akigundulikan ana hatia, huenda asikabiliwe na mashtaka kwa vile kihistoriea msimamo wa Wizara ya Sheria umekuwa kutowashtaki marais walio madarakani.