"Hii ndiyo heshima kuu zaidi kuwahi kutunukiwa katika maisha yangu yote," alisema Kindiki katika uwanja wa KICC mjini Nairobi.
"Ningependa kuhakikishia Wakenya na Rais Ruto kwamba nitahudumu kwa uaminifu," alisema katika hotuba yake.
Hafla ya kuapishwa kwa Kindiki iliongozwa na msajili mkuu wa mahakama Eilfridah Mokaya Boyani.
Bunge la Seneti lilipiga kura ya kumuondoa Naibu Rais wa wakati huo Rigathi Gachagua afisini mwezi Oktoba kutokana na mashtaka yakiwemo ukiukaji mkubwa wa katiba na kuibua chuki za kikabila, shutuma ambazo anazikataa na amezipuuza kuwa zimechochewa kisiasa.
Mahakama Kuu ya Kenya ilisitisha kuapishwa kwa Kindiki baada ya Gachagua na wafuasi wake kuwasilisha kesi zaidi ya 30 za mahakama kuzuia kuachishwa kazi kwake na kujazwa kwa nafasi yake.
Lakini agizo la kuzuiwa liliondolewa Alhamisi, huku majaji wakisema kuwa nafasi ya naibu rais haipaswi kubaki wazi kwa mujibu wa katiba.
Changamoto za kisheria za Gachagua ziliongeza miezi kadhaa ya misukosuko ya kisiasa nchini humo, ambayo ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki, ambayo ilianza na maandamano ya nchi nzima kupinga nyongjumuisha wanachama wa upinzani katika baraza lake la mawaziri kuunda kile alichokiita serikali ya umoja mwezi Julai ili kujaribu kupunguza hali ya wasiwasi baada ya waandamanaji kuvamia bunge.
Mabailiko hayo ya kisiasa pia yalimweka kando Gachagua, ambaye alikuwa na umuhimu mkubwa wa kisiasa kwa Ruto wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, na kusaidia kupata kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la Mlima Kenya.
Kindiki aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi baada ya rais kuchukua madaraka Septemba mwaka huo.
Alhamisi Ruto alimteua mkuu wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi kama kaimu waziri wa mambo ya ndani, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Kindiki hapo awali.