Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:46

Kenya kumuapisha naibu rais mpya Ijumaa Nov 1


Naibu rais mteule Prof Kithure Kindiki.
Naibu rais mteule Prof Kithure Kindiki.

Mahakama kuu nchini Kenya imeondoa amri iliyokuwa imewekwa kuzuia kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki kama naibu rais wa Kenya.

Jopo la majaji watatu Eric Ogola, Anthony Mrima na Fredah Mugambi, wamesema kwamba amri iliyokuwa imetolewa na mahakama kuu ya Kerugoya imeondolewa lakini wakasema waliofungua kesi wana haki ya kukata rufaa.

David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walikuwa wameomba mahakama kuzuia kuapishwa kwa Kindiki baada ya bunge kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kuwa naibu rais baada ya Senate kumuondoa ofisini Righathi Gachagua.

Mathenge na Kamotho walifungua mashtaka dhidi ya senate, spika wa senate na wengine wawili.

Majaji wamesema kwamba kesi ya Gachagua kupinga kuondolewa ofisini itasikilizwa kuanzia Novemba 7. Imesema kwamba Gachagua ana haki ya kukata rufaa.

Matayarisho ya kuapisha Prof Kindiki

Mkuu wa watumishi wa uma Felix Kosgei ameunda kamaji ya watu 23 na majina yao yamechaoikwenye gazeti rasmi la serikali. Kamati hiyo ina jukumu la kutayarisha sherehe ya kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki kama naibu rais wa Kenya.

Kamati hiyo itaongozwa na katibu mkuu wa baraza la mawaziri Mercy Wanjau. Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor ni mmoja wa wanachama kwenye kamati hiyo, pamoja na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Raymond Omollo.

Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ametangaza kesho Novemba 1 kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki.

Forum

XS
SM
MD
LG