Kesi ya kwanza ya uhalifu inayomkabili Trump kuanza wiki hii New York

  • VOA News

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Kesi hiyo kuhusu Donald Trump kutoa fedha kulipwa mwanamke mmoja itaanza leo Jumatatu kwa kuchagua jopo la mahakama.

Katika tukio jingine, Rais Joe Biden, ambaye anawania kuchaguliwa tena, atakuwa katika kampeni yake huko Pennsylvania.

Rais wa Marekani Joe Biden

Jimbo lenye ushindani mkali la Pennyslvania lilikuwa la mwisho la kampeni ya uchaguzi kwa Donald Trump kabla ya kesi yake ya “kutoa pesa” leo Jumatatu huko New York.

Anakabiliwa na makosa ya jinai 34 kwa kugushi rekodi ya biashara, akituhumiwa kuficha pia mahusiano yake na mcheza filamu za ngono Stormy Daniels mwaka 2006.

Wakati wa mkutano wa Jumamosi huko Schnecksville, mgombea urais mtarajiwa wa Republican kwa mara nyingine amezungumzia kesi yake ni kumtafuta mchawi.

Rais Donald Trump, Mgombea Urais Mtarajiwa, Mrepublican anasema: “Kesi zote ni za Biden, mnajua hilo, sawa? Najivunia kuwafanyia nyinyi. Muwe na wakati mzuri kuangalia.”

Kwa vile hii itakuwa ni kesi ya kwanza ya jinai ya rais wa zamani, kesi kwa hakika itafuatiliwa kwa karibu sana… amesema mchambuzi wa siasa Calvin Dark.

Calvin Dark, Mchambuzi wa Siasa anasema: “Naamini hadi hivi sasa, majaji kwa kiasi kikubwa na waendesha mashtaka wamefanya kazi nzuri sana katika kujaribu kuhakikisha kwamba jinsi anavyotendewa Trump anapewa kila linalowezekana kama Mmarekani wa kawaida angetarajia kama wangekuwa katika hali kama hiyo.”

Akionekana katika kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week”, gavana wa New Hampshire, Mrepublican Chris Sununu, amesema hatarajii kuwa kesi hiyo maarufu kama ‘hush money’ itakuwa na athari kubwa za kisiasa kwa Trump.

Chris Sununu

Chris Sununu, Gavana wa New Hampshire anaeleza: “Kwa hakika watarejea kwenye kampeni na kuelezea kile ambacho kinaendelea; watajaribu kuonyesha kudhulumiwa na hiyo limefanya kazi kwake.”

Mtizamo wa Rais Joe Biden, wakati huo huo, umekuwa ni kujihusisha kikamilifu katika … Kujibu shambulizi la Jumamosi la Iran kwa Israel,

Lakini pia alitarajiwa kufanya kampeni zaidi wiki hii….. Atakuwa Pennyslvania kwa siku tatu. Suala kuu atakalolizungumzia: uchumi.

Karlyn Bowman, American Enterprise Institute amesema: “Atazungumzia kuhusu ukweli kwamba kuna baadhi ya ishara ya kuboreka kwa uchumi, ingawaje mfumuko wa bei wiki iliyopita haikuwa nzuri kwa utawala.”

Suala jingine ni kwamba kampeni ya Biden imekuwa ikiboreka na huenda ikaendelea kulenga katika wiki hii ulinzi wa haki za uzazi, hasa baada ya Trump kusema wiki iliyopita kwamba uamuzi wa kutoa mimba uachwe ufanywe na majimbo.