Mapumziko ya siku ya kumbukumbu ya taifa ya Martin Luther King itakayo adhimishwa Jumatatu itawapa wajumbe hao muda huo wa kutafakari.
Baraza la Seneti limepeleka wito kwa Trump Alhamisi, likimjulisha juu ya kesi hiyo na mashtaka yanayo mkabili. Ni lazima ajibu wito huo kwa maandishi ifikapo Jumamosi jioni.
Kesi ya Trump yakutaka kumuondoa madarakani imekuja wakati kuna mpasuko mkubwa wa kisiasa nchini na imekuja wakati Wademokrat, wakiwemo maseneta kadhaa, wakiwa wanagombea kinyang’anyiro cha nafasi ya urais dhidi yake katika uchaguzi wa rais unaokuja.
Taasisi inayofuatilia masuala ya serikali ilijumuisha Alhamisi kuwa Trump alivunja sheria ya matumizi ya serikali mwaka 2019 wakati alipositisha kwa muda matumizi ya dola za Marekani milioni 391 zilizokuwa zimepitishwa na bunge kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Kadhalika waangalizi hao wamesema Trump alishinikiza Kyiv kuanzisha uchunguzi ili kujinufaisha yeye mwenyewe. Uamuzi huo unajikita katika kiini cha kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya kiongozi huyo wa Marekani.